Kampuni ya Pernod Ricard kupitia kinywaji chake cha-
Jameson Irish Whiskey iliandaa hafla maalum ya kuonjesha kinywaji chake katika mgahawa
wa High Spirit Lounge, jijini Dar es salaam jana.Hafla hiyo iliandaliwa na Balozi wa Jameson Kanda ya Afrika- Nelson Aseka.
Bwana Aseka, ambaye amepewa mafunzo maalum kutoka kwa wataalam wa kinywaji cha Jameson Irish
Whiskey nchini Ireland na mwenye miaka mingi kuwa Balozi wa kinywaji hich alisema, “Jameson
inaongoza duniani kwa mauzo katika kitengo cha whiskey kutoka Ireland na imeanza kupata
umaarufu nchini Tanzania.
Sababu kuu ya Jameson kuongeza umaarufu wake ni kupitia mbinu
zinazotumiwa katika utengenezaji wa kinywaji hiki ambayo inaipa ladha nzuri zaidi. Jameson imezidi
kupata ongezeko la mauzo na ubora kwa miaka 24 sasa na inatarajia kuendeleza jambo hili kwa
kuingia katika soko la Afrika Mashariki”.
Naye Meneja Ukuzaji Bidhaa wa Pernod Ricard, Bwana Adam Kawa alisema, “ Hii ni moja kati ya
hafla nyingi ambazo Pernod Ricard itaandaa katika soko la Tanzania na sio tu kwa kinywaji cha
Jameson bali kwa vinywaji vingine kama vile: Ballentine’s, Absolut Vodka, Chivas, Beefeater na
Malibu. Na kama mlivyoona katika hafla ya leo tutaendelea kuwafanyia wateja wetu hafla
zinazowapatia uzoefu zaidi juu ya bidhaa zetu”.

Balozi Mkuu wa kinywaji cha Jameson Whisk, Nelson Aseka akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywaji hicho na jinsi namna
kinavyotengenezwa.Hafla hiyo iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini
Dar es Salaam.

Meneja masoko wa Jameson Whisk,Adam Kawa akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywa hicho iliyofanyika katika mgahawa wa
High Spirit jijini Dar es Salaaam.


Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika hafla ya kuonja Jameson Whisk iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...