Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale ametangaza kuanza rasmi kwa majaribio ya kupima magari kwenye Mzani wa Kisasa wa Vigwaza mkoani Pwani ambapo majaribio hayo yataendelea hadi siku ya tarehe 17/03/2015. 
Kwa mujibu wa Eng. Mfugale, mara baada ya majaribio kukamilika siku hiyo kituo cha Mzani wa Kibaha katafungwa rasmi na magari yataendelea kupimwa kwenye kituo kipya cha Vigwaza ambacho kina uwezo wa kupima gari moja likiwa linatembea kwa muda usiozidi sekunde 30 tofauti na mzani wa zamani uliokuwa unatumia dakika moja na nusu. 
Eng. Mfugale amewataka madereva kufata taratibu zifuatazo katika Mzani huo mpya utakaokuwa unapima magari yakiwa kwenye mwendo yani weigh-in-motion i) Magari yanayotakiwa kupimwa kwa mujibu wa sheria ni yote yanayoanzia tani tatu na nusu.(3.5) Magari yanatakiwa yaendeshwe kwa kupita upande unaostahili kisheria yaani hayatakiwi kukanyaga mstari mweupe katika barabara.
Eng. Mfugale aliongeza kuwa usipofata utaratibu huu katika Mzani taa nyekundu mbele ya itawaka na dereva kuelekezwa kwenye mzani mkubwa hata kama hujazidisha uzito na utatakiwa kulipa tozo la dola za Kimarekani 2000 kuashiria kwamba dereva anakwepa mzani. 
Eng. Mfugale alisema kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya Usalama Barabarani namba 30 ya mwaka 1973 na kanuni zake za mwaka 2001 kifungu namba 6(b) ii) Madereva wanatakiwa wazingatie mwendo wa kilomita 50 kwa saa iii) Madereva wahakikishe kuwa matairi ya magari yao yanapita juu ya plates za weigh-in motion na kuachana mita 30 yanapokaribia kupita eneo la Mzani ili kuondoa usumbufu wakati wa upimaji 
 Pia Eng. Mfugale ametoa angalizo kuwa gari lolote litakalozuia magari mengine kwenye barabara ya maingilio ya Mzani au kwenye mzani wakati wa upimaji kutokana na ubovu wa magari hayo yatatozwa faini kiasi cha Tsh. 300,000/= au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja na hiyo ni kwa mujibu wa kifungu 50(1) (f)(g)(h)(i) cha Sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007. 
Mwisho Eng. Mfugale amewashauri wamiliki wa magari kuhakikisha kuwa madereva wao wanakuwa na wasaidizi watakaowasaidia kupeleka nyaraka za gari na mzigo ili kurekodiwa kwenye ofisi za mzani. 
Mzani wa Vigwaza ni wa kwanza kujengwa nchini na una uwezo wa kuchambua na kubaini magari Weigh-in- Motion yaliyozidisha uzito huku yakiwa yanatembea. 
 Pia kituo hicho cha Vigwaza kina Mzani mkubwa multi deck wenye uwezo wa kupima gari lolote kwa mkupuo. Pia barabara za kuingia kwenye mzani mkubwa zenye urefu wa km 1.8 zimejengwa kwa zege lenye uwezo wa kudumu kwa miaka 50. Picha na Stori kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi
 Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akiwaonyesha Waandishi wa Habari namna ya upimaji wa magari katika Mzani mpya wa Vigwaza ambao umeanza kufanya kazi kwa majaribio.
Magari yakiwa yameanza kupima kwenye Mzani mpya na wakisasa wa Vigwaza. Mzani huu unapima gari moja kwa muda wa sekunde 30 tofauti na Mzani wa zamani wa Kibaha uliokuwa unatumia dakika moja na nusu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ila Tanzania mitandao mingine inatoa habari za uwongo na kuwapotosha watu. Fb kuna mtando umesema mizani hii imeharibika na kuonesha barabara yake kudidimia, hatuelewi tushike lipi. leo hapa michuzi anatuonesha mzani uko pouwa sasa sijui lipi tusifie na lipi tupuuzie Michuzi!

    ReplyDelete
  2. Tatizo Tanzania siku hizi kila anaeweza kukaa mbele ya keybord tayarri anakuwa mwanahabari,mwanasiasa,mwanasheria, kocha yaani alimradi tabu.tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...