Kampuni inayoongoza kwa huduma ya teknolojia ya mawasiliano, Push Mobile Media imezindua huduma ya ujumbe kwa njia ya mtandao wa internet ijulikanyo kwa jina la “Bulk Messaging” kwa lengo la kumwenzesha mtumiaji kufikisha ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kufikisha ujumbe muhimu kwa gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali na kwa mtu binafsi.

Manento alisema kuwa lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na sekta nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na kujitangaza.

“Kama ni mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa muhimu utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo ya biashara zao,” alisema Manento. “Ili kupata huduma hiyo, unatakiwa kujiunga kupitia mtandao wetu, www.pushgw.com na kufungua akaunti yako,” alisema Manento.

Alisema kuwa makampuni au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa wafanyakazi, wateja wao kuhusiana na biashara na taarifa nyingine. “Kwa watu binafsi, unaweza kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na harusi na hata kwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la kuwasiliana na wahariri wao kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,” alisema.

Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi alisema kuwa huduma hiyo ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe kwa kiasi cha sh 16 kwa kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.

Alisema kuwa kwa upande wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na madaktari kuwakumbusha wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu. “Unachotakiwa kufanya ni kujiunga na huduma hii kwa njia ya mtandao na kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa na kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo kuhusiana na huduma ya ‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi (Kulia) akielezea umuhimu wa huduma ya “online bulk Messaging’ kwa sekta mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ufundi.
Mkuu wa Idara ya Ufundi wa Kampuni ya Push Mobile Media Daniel Buchafwe akielezea jinsi ya huduma ya “online bulk messaging” inavyofanyakazi. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...