Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Bwa.Israel Elly Nawinga mapema leo asubuhi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,Pichani kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai,Mh Anthony Mtaka.Bwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage Nyerere.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tisa ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama cha CCM ya mwaka 2010 ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi
Bwa.Israel Elly
Nawinga akiuzungumza jambo na Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo asubuhi alipopita kumsabahi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai
mkoani KilimanjaroBwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya
Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage
Nyerere.
PICHA NA MICHUZI JR-HAI MKOANI KILIMANJARO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...