Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka
zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo,ambalo
lilikuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na barabara ya eneo hilo kulika
na mmomonyoko wa udongo.
Ujenzi wa daraja la Kisongo ukiendelea kwa kasi,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wake.
Baadhi ya wananchi wa Kisongo wakipita juu ya barabara ambayo imeanza kuathirika na mmomonyoko wa udongo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege
wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire,ujenzi wa kituo hicho
unatarajia kuisha mwaka huu ambapo kiasi cha fedha zaidi ya shilingi
milioni 500 zitakuwa zimetumika kukamilisha ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya
makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebe
msalaba wake.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye
akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa
Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi
wananchi.Ndugu Kinana wa pili kushoto alikuwepo kusikiliza malalamiko
hayo na kuwapatia majibu.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa
sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.
Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo,Said Mwishehe akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika ndani ya jimbo la Arumeru Magharibi,pichani shoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza.Ndugu Kinana yupo kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
PICHA NA MICHUZI JR-ARUMERU MAGHARIBI ARUSHA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...