Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli,Amani Ole Torongei,akizungumza jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku akionesha fulana ya CHADEMA akieleza kuwa amechoka kuwa mtumwa.Amani alitangaza kukihama chama chake na kutangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho cha CCM.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa wilaya ya Ngorongoro kupitia chama cha CHADEMA,Revocatus Mpalampala,akizungumza jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.Revocatusi alitangaza kukihama chama chake na kutangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho cha CCM.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi Kata ya Olorien,mkoani Arusha kupitiaa chama cha CHADEMA,Prosper Mfinanga akivua sare za chama chake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo,akiashiria kukihama chama hicho na kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hivyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake katka mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.Ndugu Kinana akiwa emeambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wajumbe wengine leo wanahitimisha ziara ya siku nane mkoani humo ya Kuhimiza,kukagua na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Ndugu Kinana katika ziara yake ndani ya mkoa wa Arusha ametembea umbali wa kilometa 2671,Wilaya zote sita za mkoa huo yakiwemo na majimbo saba ya uchaguzi.Amefanya mikutano 69,mikutano nane ya ndani na mikutano 61 ya nje kwa kuzungumza na Wanachi kuyasikiliza matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.Kama vile haitoshi Ndugu Kinana ametembelea miradi 49,miradi sita ya CCM katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi na miradi 43 ya serikali.
Katika taarifu fupi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kuhusiana na wanachama wapya,ziara hiyo imejiongezea wanachama wapya wapatao 4290,ambapo wanachama 519 kutoka CHADEMA walijiunga na chama hicho cha CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,wakati wa kuhitImisha ziara yake ya siku nane ndani ya mkoa huo.
PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA
njaa tu zinawasumbua na waende kwenye chama chao kipya..watuache tuendelee na ukombozi wa maskini
ReplyDeleteSio ukombozi wa masikini ni ukombozi wa wachaga hahahahaaaaaaa mmemuondoa zitto makusudi mbaki na vilaza mnaoweza kuwaongoza kwa mbwembwe na mtakavyo sasa muda wenu umewadia nchi hii itaongozwa kwa misingi ya haki na utawala bora baada ya peoples power nyie mmefanya parties power poleni wakuu.
ReplyDeleteWanahamahama kwa kuwa ni wachumia tumbo! Ni kuendekeza njaa tu.
ReplyDelete