Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikatiza kwenye moja ya mtaro alipokwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa. Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Pichani
Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongoza na Mkulima
bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa na Mumewe pichani kulia,ambapo Ndugu
Kinana alikwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima
huyo katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu kushoto) akishiriki kulima shamba la
karanga la Mkulima bora wa mwaka 2014 mkoa wa Dodoma,Bi.Anna Mlewaka
katika kijiji cha Berege Wilayni Mpwapwa mkoani Dodoma.Mkulima huyo
alieleza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuwa 2012/13
alifanikiwa kulima ekari 30 na kuzalisha kiasi cha gunia 300 za
mtama,mnamo mwaka 2014 alihamasika kuongeza eneo kufikia ekari 130
ambazo alizalisha gunia 650.Mkulima huyo alisema kuwa mpaka sasa
amefanikiwa kununua power tiller 1,ameanzisha biashara ya duka na
mashine ya kusaga,anasomesha watoto shule ya msingi,sekondari na chuo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuiarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Wakazi wa Mpwapwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-Taifa,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni .
PICHA NA MICHUZI JR-MPWAPWA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...