Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe (kushoto),
akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Mwakilishi Mkuu wa zamani wa
Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Yasunori Onishi, ofisini kwake jijini
Dar es Salaam mara baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi
nchini.Mwakilishi huyo ameishukuru Wizara ya Ujenzi kwa ushirikiano
aliopata katika kipindi chote alichohudumu nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe (kushoto),
akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkuu mpya wa Shirika la Maendeleo la
Japan (JICA) Toshio Nagase (kulia) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe akifurahi jambo na
Ujumbe kutoka wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wakati ugeni
huo ulipotembelea ofisini kwake kwa lengo la kutoa pongezi za JICA
kwa Wizara ya Ujenzi kutokana na utekelezaji mzuri wa miundombinu
ya barabara.Picha na Habari kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
---
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe amelipongeza
Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA) kwa ufadhili wa miradi
mingi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara iliyokamilika na inayoendelea
nchini.
Eng. Iyombe ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati
akiagana na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Bw. Yasunori Onishi, ambae
amemaliza muda wake na kumpisha Mwakilishi Mkuu mwingine Bw.
Toshio Nagase.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...