Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Jaji Mkuu Nchini Othman Chande amesema kesi za mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)zinatakiwa kufanywa kwa ushirikiano katika pande zote ikiwemo mashahidi kujitokeza kwa wakati kwa watuhumiwa wa mauji hayo.
Jaji Chande ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuapishwa Manaibu wa Usajili wa Mahakama Kuu leo jijini,Dar es Salaam,amesema watu wenye ulemavu wa ngozi ni watanzania wenzetu na hakuna anayependa wanavyofanyiwa ukatili huo.
Chande amesema mashahidi wakijitokeza kwa wakati,inarahisisha kwa watu wa mahakama pamoja na waendesha mashitaka kushughulikia kesi za mauji hayo na sheria itashika mkondo wake.
“Suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi linamgusa kila mtu ni uhalifu wa hali ya juu kila taasisi linagusa ,hivyo taasisi zijiandae mwaka jana zilikuwa kesi 90 ambazo zilikuwa za mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemvu wa ngozi”amesema Jaji Chande.
Aidha alisema kesi za mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi zitapewa kipaumbele,zinatakiwa zifanyike na mashahidi wajitokeze na sio wa kufichana.
Alisema muundo mpya wa mahakama umetenganisha majukumu ya watendaji na wasajili wa mahakama kuu na rufani na kuwa Manaibu wa wasajili ndio watafanya kazi za kiusajil kesi pamoja na kusaidia uendeshaji wa kesi.
Alisema majukumu ya Manaibu wa wasajili wa mahakama kuu na rufani ni urahishaji wa kalenda ya mahakama ,kuainisha gharama za mawakili,kusikiliza kesi za mauaji ,pamoja na utafutaji wa madalali.
Chande alisema wanatarajia kuajili watendaji 111 katika mahakama za wilaya zote nchini ,nakala za hukumu zitatolewa kutokana ni haki yao ya watu kupata nakala hizo .
Huu utakuwa msaada mkubwa muheshimiwa.
ReplyDelete