Angelina
Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania ,
Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha
Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi
Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na
OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu
mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi,
Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa
kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake
kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo.
Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo
Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia
wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
Mmoja
wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi
akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii
kwa ujumla.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...