Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Manzase Kata ya Fufu wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia leo jioni katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Manzase,Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, yupo katika ziara ya mikoa mitatu Dodoma,Arusha na Kilimanjaro ya kuhimiza,kukagua Ilani ya CCM ya mwaka 2010 na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapati ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia baadhi ya wakazi wa kijiji cha Manzase kata ya Fufu,,jimbo la Mtera wiyani Chamwino mkoani Dodoma,leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akishihudia tukio hilo adhimu. Kinana amelishukuru shirika hilo kwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa kisima hicho kwa muda mfupi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa wilaya na mkoa wa Dodoma wakikagua mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Suli yaliyogharamiwa na shirika la Neigbourhood kutoka Korea ya Kusini,kwa kiasi cha shilingi bilioni tatu,ujenzi huo pia unahusisha vyumba vya walimu pamoja zahanati ya kijiji cha Suli.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutanno huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino jioni ya leo.
PICHA NA MICHUZI JR-MTERA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...