Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu hoja mbali mbali zilizoletwa na kamati ya soko la Kilombero ikiwa pamoja na kupandishiwa kodi bila utaratibu maalum.Ndugu Kinana anatarajia kuhutubia kesho katika mkutano wa hadhara ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Arusha kwenye soko la Kilombero ambapo walisalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi.
Wananchi na Wafanyabiashara mbalimbali katiko soko la Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao ikiwemo pia na kuyasikiliza matatizo mbalimbali yanawakabili katika soko hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali wakila chakula kwa Mama Lishe wa soko la Kilombero,jijini Arusha,pichani kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana,Mh.Catherine Magige.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakinywa kahawa mara baada ya kumaliza kuwasalimu na kuzindua shina la wakereketwa wajasiliamali Oysterbay, Unga ltd, Arusha.
PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...