Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akiwa amebeba maji kwenye madumu aliposhiriki
umwagiliaji maji katika shamba la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM
katika Kijiji cha Nkulabi, Kata ya Mpunguzi, Jimbo la Dodoma Mjini leo
wakati wa ziara yake,Kinana yupo mkoani Dodoma kwa
ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,
kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi pamoja
na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimwagilia maji zao la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Mpunguzi, Dodoma. Kinana aliwapongeza vijana hao wanne kwa kuamua kuanzisha shamba hilo ambalo mazao yake yanawasaidia kujikimu kimaisha.Kinana aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Dodoma, ambapo ametoa ushauri kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kuwasimamisha mara moja watumishi wanaotajwa kwenye sakata la Escrow kama CCM ilivyowasimamisha viongozi watatu waliotajwa kwenye sakata hilo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Barafu,Nape aliwaambia wakazi hao kuwa makini na wapinzani kwani wamekuwa wakihangahika na fedha za wafadhili ambazo hawaitakii mema nchi yetu.
Pichani ni baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.
PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
Kinana sasa KILIMO KWANZA inayojumuisha maji ya mifereji, mabwawa, mbolea, matrekta, masoko ya uhakika, viwanda vya kusindika mazao kuongeza thamani kwa mkulima lini yatatimizwa?
ReplyDeleteMaana hizi harakati za kutumia misuli zitakuumiza Mzee wetu tafuta namna KILIMO KWANZA kilete Matokeo Makubwa SASA.
Mh kinana unafanya kazi Nzuri sana upande wa chama ila unaangushwa upande wa serikali kwa kweli.
ReplyDeleteUsanii ni kazi vilevile
ReplyDeleteWatumie Drip Irrigation. Hata vijana hao wakibeba maji mabegani Kilimo watakiona kuwa ni adhabu.
ReplyDeleteTeknolojia bado ni ndoto Tanzania. Kwa kubeba maji namna hii utalima hekari ngapi? au tunazungumzia kulima chakula cha familia yapo peke yake??
ReplyDeleteKinana akimaliza hizi hekaheka lazima achukue likizo ya miaka miwili apumzishe mwili.
ReplyDelete