Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania mapema leo asubuhi katika ukumbi wa White House,mjini Dodoma.Ndugu Kinana amewataka wasomi hasa wanafunzi wa vyuo vukuu nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za juu za chama hicho.

Kinana amesema kuwa chama cha mapinduzi CCM kimejipanga kutumia vijana hasa wasomi kwa kuleta changamoto mpya ndani ya chama hicho,ambapo amewatoa hofu ya kushiriki kwenye siasa hata kama hawana fedha na kuwa kujaribu si kushindwa na watakuwa wamejitambulisha kwenye majukwaa ya siasa na kutoa mifano kwa baadhi ya vijana ambao walijaribu na siku ya mwisho waliibuka washindi kwa kuwabwaga baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho na serikalini wakiwemo madiwani.
 Baadhi ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakishangilia jambo ndani ya ukumbi wa wa White House kabla ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuzungumza nao mambo mbalimbali.
 Mkutano ukiendelea ndani ya ukumbi wa White House mjini Mdodoma.
Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa akiwa pamoja na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Bi Fatuma Mwenda pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Betty Mkwassa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana nje ya ukumbi wa White House mapema leo asubuhi.Nduugu Kinana anaendelea na ziara yake wilaya ya Dodoma mjini na vitongoji vyake.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma,Mh.Betty Mkwassa.

PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...