Katika kile kinachooneka na ni kujipanga vyema, kampuni gwiji la mawasiliano duniani Huawei imeanza kutangaza kuja na kitu kipya na kikubwa zaidi hivi karibuni.  Tunaweza kusema huu ni mwaka wa Huawei, au tuseme huu ni msimu wa Huawei kufanya yao kwani ni mwezi huu huu wamezindua bidhaa kali na tumeanza kusikia minong’ono ya kuwa ku na mengine yanakuja.  

Tofauti na tulivyozoea kuwa wanatangaza uzinduzi wa bidhaa ila sasa hivi wanakuja na “kishkwambi”. Hakuna ajuaye kishkwambi ni nini kwani inaweza kuwa ni bidhaa mpya au inaweza kuwa ni zawadi kwa wapenzi wake laki ni inaonekana wazi kuwa ni jambo kubwa.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii, Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo alisema kuwa ‘kishkwambi’ ni habari ya mjini, maalumu kwa wapenzi wao na kuwaomba watanzania wote watembelee kurasa zao za mitandao ya kijamii kujua zaidi pia tovuti maalumu ya kishkwambi hapahttp://huawei.kishkwambi.co.tz/
Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake nchini China, imekuwa mstari wa mbele kufikisha teknolojia ya kisasa kwa watu duniani kote. Kwa hapa nchini wamekuwa wakitoa simu za bei nafuu na hivyo kufanya watanzania wengi kupata teknolojia hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...