Kumbukizi maalum ya tarehe 20 Machi 2015 ya wanafunzi watano wa Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani
imetukumbusha msiba mkubwa wa watu 50 katika ajali moja ya basi na lori ya
tarehe 11 Machi 2015.
Wakati tukiendelea kuwaombea marehemu na majeruhi na kutoa pole kwa wafiwa
na wahanga wakati umefika sasa tutangaze #AjaliBarabaraniJangalaTaifa
tuwajibike kuzipunguza.
Kumbukizi katika ukumbi wa Nkurumah ilihusisha ibada, nyimbo maalum na
kusomwa kwa wasifu wa wanafunzi walioaga dunia wakiwa wadogo familia zao
na taifa likiwahitaji na hatimaye salamu kutoka makundi mbalimbali.
Niliguswa na salamu za Chuo cha Fani za Jamii zilizosomwa na Mkuu wa Chuo
cha Fani za Jamii aliyeeleza kwamba mabasi sasa yanaua kuliko magonjwa mengi.
Alipendekeza utafiti ufanyike UDSM kuchangia kupunguza hali hiyo kwa
kuzingatia kwamba Chuo Kikuu hicho kina fani mbalimbali (multi disciplinary).
Alieleza kwamba kwa upande wa uhandisi waangalie iwapo teknolojia ya mabasi
yenye spidi inawiana na barabara zetu kuu ambazo nyingi ni za njia moja. Huku
fani ya jamii iangalie masuala ya maadili kufanya madereva wa mabasi kujifunza
kwamba wanabeba binadamu sio wanyama.
Ile ajali inauma sana mpaka leo na kesho. Usiambiwe na usiombe ukutwe na janga kama hilo awe ndugu yako au mzazi or rafiki hata mtu yeyote. Jamani ile ajali inaniuma roho. Sielewi shetani gani asiyesikia sala na maombi ya watu anaangamiza watu kiasi hiki. Ila Mungu anaona na anajibu maombi tuzidi kusali kuombea usalama wa abiria wetu.
ReplyDelete