Na Henry Mdimu
Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. 
Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea. Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. 
Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili  na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi. 
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi? Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu. Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa? #IMETOSHA
 Bango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino. 
Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"
 Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine 
Rafiki wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Unatafuta mtaji kumbe?! alafu ni zoezi lako? Jamani jamani isije watu wakawa wanatafuta mitaji na utajiri kupitia ili swala!

    Cha kufanya:

    (1) Kusiwe na Vikundi vingi huku kila mtu akitaka kufungua vikundi vipya kila siku kwa ajili ya kujinafsisha nafsi zao kwa njia moja au nyingine bali tunabidi kuwekeza nguvu kwa kikundi kimoja kitachowakilisha jamii hii na kupeleka ujumbe katika kila pembe ya Tanzania.

    (2) Serikali itangaze hali ya maafa nchi nzima (hali ya dharura) kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ili Serikali iweze kuwalinda, Kujenga maeneo maalumu (Disaster Recovery Centers), kutoa elimu kwa njia ya TV, Radio, Magazeti na vijarida na pesa hii yote itoke ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha maafa na pesa ipelekwe katika kila Mkoa na Kila kitongoji. Kama tunafanya hivi kwenye mafuriko basi hatuwezi kushindwa kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.

    (3) Serikali ishirikiane na Mashirika ya Kimataifa pamoja na Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS) kulivalia njuga ili swala na kulitokomeza mara moja. Serikali iunde tume chini ya Mwenyekti wake atakae teuliwa na Mh Rais, tume itakayochunguza na kubaini mtandao mzima wa wahusika.

    (4) Mbali na hii tume hapo juu, Jeshi la Polisi ikishirikiana na Idara Ya Usalama wa Taifa iweze kufanya kazi 24/7 kuweza kutambua mtandao mzima na kuwatambua wanaowahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria. Nina uhakika zaidi ya asilimia 100 kwamba Idara Ya Usalama wa Taifa ina uwezo mkubwa saana kulibaini ili swala mapema sana.

    Asanteni na naomba niishie hapa na kuwapa fursa wengine kuchangia.

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki watu wake.

    ReplyDelete
  2. Good job guys,

    ReplyDelete
  3. Why some people are mean like that? God will punish them

    ReplyDelete
  4. Mjomba umetiririka vizuri sana ni kweli isije ikawa ni kiji Mradi cha wachache!

    ReplyDelete
  5. Tunazidi kulaani kitendo hiki kilichotokea kwa mtoto Baraka hata hawa waliohusika watafutwe wasipate mahali pa kujificha.

    ReplyDelete
  6. "Imetosha" That is a wrong message. Yaani kizungu ni kama kusema enough is enough au kiarabu, kifaya.Kitendo hiki needs to be condemmed outright not just because mpaka sasa "IMETOSHA" yaani ukatili mmaotupa hadi hivi, sasa imetosha.
    Ankal I may have misread this but let wadau wanifunulie tafsiri

    ReplyDelete
  7. Huu ni mradi wa watu dalili zote zinaonesha waziwazi kwamba watu wanataka kupigwa changa la macho hapa.

    Picha ndio limeanza ngoja tuone litakavyoisha.

    ReplyDelete
  8. Yaani hii aibu ya Tanzania hata sura tunashindwa kuzificha. Wametoka kanda ya ziwa wamekuja kusini magharibi jamani? Ewe Mungu tunaomba uwalinde watu wako. Ipo siku mambo haya yatapata ufumbuzi tu. Na hao wanaofanya mambo haya arobaini yao yaja. Machozi na vilio vya watanzania wengi hayataenda bure. Mola wetu utusikie.

    ReplyDelete
  9. Mbona tangu haya mauaji yameanza hakuna OCD wala DSO, Mwenyekiti wa mtaa au kijiji hata mmoja aliyejiuzuru? Mbona wakati ya mauaji ya Shinyanga miaka ya 1970 Mzee Mwinyi na Mrema waliachia ngazi. Je kujiuzuru mpaka iwepo kashfa ya rushwa tu je maisha ya ndugu zetu wenye Albinism hayana thamani kuliko ufisadi mdogo au mkubwa.

    Tunaomba sasa iwebasi mauji yajitokea tena basi tunaomba OCD, DSO na Mwenyekiti wa Kijiji au mtaa na serikali yake wote wawajibike. Tatizo hili litakwisha. Linaendelea kujitokeza kwasababu inaonekana kuwa wanaweza kufanya hayo matukio na sheria haina makali ya kuwakata au kuwawajibisha. IMETOSHA.

    ReplyDelete
  10. Anon wa Kwanza umeyasema yote tunayowaza wengi. Asante sana.
    Kwa nini makundi mengi ? Mpaka inafikia wanaenda kupigana ngumi nje ya Ikulu ? Na cha kusikitisha zaidi hili tatizo ni kubwa sana lakini jinsi Kampeni za makundi tofauti zinavyoendeshwa ni kama Watu wanatafuta ulaji zaidi na si vinginevyo. Kwa maana kampeni zinafanyika Mjini wakati tatizo liko Vijijini, ambako hamna hata Television za watu kujua kwamba leo "Imetosha" ilikuwa inafanya kampeni. Ili tatizo hili la mauaji ya Albino liwe Historia kuna Ulazima wa Makundi yote husika kujipanga na Kufanya Kazi kwa Pamoja
    . Haya labda tusubiri kile Kikosi Kazi kilichoundwa kwa pamoja na Serikali na Chama cha Albino kikafanye kazi huko kwenye chimbuko la tatizo kitaleta suluhishi. Maana mpaka sasa ndio Kikosi pekee kinacholeta matumaini kwa kuwa kimeamua kulifuata tatizo huko liliko na si kukaa mjini kutafuta Umaarufu. POLENI SANA WAATHIRIKA WOTE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...