MASHEIKH wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.MSIKILIZE HAPA.

Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu,"alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za Elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii. 
Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.
 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Masheikh inakuwaje wanachnganya dini na siasa?! haitungii akilini kuwa mashekh wamuchangie laki 7 Mhe.Lowasa kwa ajili ya kugombea uraisi ? huu ni mchezo wa kuigiza kweli,kama masheikh wanafedha hizo kuna vyuo au madrasa ngapi hazina ata paa,mbona hakuna hata hosptali nyingi sa kiislam? misiki mingapi haiko katika hali mabaya na majengo yake? Leo mnauwezo wa kumchangia mwanasiasa kugombea urais huu ni unafiki na ni mchezo wa kuigiza

    ReplyDelete
  2. Kuelekea uchaguzi tutaona mengi mwaka huu!

    ReplyDelete
  3. Mdau wakwanza hapo juu ,uko sahihi kabisaa , ila wanakuambia zakuambiwa changanya na zako ! Pembeni yuko muheshimiwa profesa juma kapuya ! Kwa ushauri wangu mimi , watanzania uchaguzi huu tujitahidi kujiandikisha kwa wingi na kuhakikisha kila mtu anachagua kiongozi atakae ona anamfaa atakaeyapatia ufumbuzi matatizo sugu katika nchi yetu ! Kila mtu aithamini kura yake si kwa pesa wala umaarufu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...