Na Bashir Yakub.
Jumatatu ya wiki hii nilianza na makala iitwayo je umeachishwa kazi au we ni mfanyakazi, zijue haki zako. Nilizungumzia masuala kadhaa yahusuyo haki za mfanyakazi. Naligusia kuhusu aina za mkataba wa ajira, muda wa mkataba wa ajira, sehemu ya kufanyia kazi, kipindi cha mpito katika kazi (probation period) na mengine mengi kuhusu ajira. Nilisema na leo tena nasisitiza kuwa ili upate ujira unaostahili ikiwa ni pamoja na mafao kwa kiwango kinachotakiwa baada ya kumalizika kwa ajira yako huna budi kuwa unajua haki zako. Usisubiri mwajiri akwambie nini unastahili isipokuwa wewe ndio umwambie mwajiri nini unastahili.
Mwajiri hawezi kukufundisha haki zako kwakuwa utazitumia kumnyima amani. Nilisema pia kuwa yawezekana unachopata na ukaona kingi sicho unachostahili kupata usipokuwa tu hujui. Kwahiyo niseme tu kwamba ni muhinmu mfanyakazi kujishugulisha kujua haki zako japo chache. Leo tunaangalia tena baadhi ya haki nyingine lakini kabla ya hapo ni ushauri.
USHAURI KWA WAFANYAKAZI.
Haki za mfanyakazi ninazoeleza hapa yawezekana wakati ukiwa kazini unaogopa kuzidai kutokana na woga wa kuonekana umekuwa mjuaji na hivyo kukaribisha uwezekano wa kupoteza ajira. Pia waweza kuwa uliacha kuzidai kwakuwa huzijui. Kama moja kati ya haya limekutokea basi ushauri wangu ni kuwa haki hizi zote waweza kuzidai baada ya kuwa umeachishwa kazi au wakati wa kustaafu kwani sheria inaruhusu. Kama hukupewa overtime,ulifanyishwa kazi muda wa sikukuu, hukupewa likizo kama inavyostahili na yote nitakayoeleza hapa chini basi baada ya kazi kuisha waweza kudai fidia yake.
1. HAKI YA KUJUA MASAA YA KAZI.
Mfanyakazi hafanyi kazi muda wote. Akifanya kazi muda wote basi uwe ni uamuzi binafsi lakini lisiwe ni agizo la mwajiri. Kazi ina muda wake na hii ni kwasababu ili mwanadamu aishi pia anahitaji kuhusika katika mambo mengine ya kimaisha nje ya kazi. Kutokana na hilo ni lazima mkataba wa ajira uoneshe masaa anayotakiwa mtu kufanya kazi. Kama ni masaa 12, masaa 8, masaa 9 yajulikane. Na ni hayo hayo tu mfanyakazi anayotakiwa kufanyia kazi. Faida ya kuainisha masaa ya kazi ni kuwa humsaidia mfanyakazi kupata malipo ya ziada iwapo masaaa yaliyoainishwa yamepita. Hii wengi wanaijua huitwa overtime. Overtime ni haki ya msingi ya mfanyakazi



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...