NA BASHIR YAKUB
Makuzi ya biashara hasa biashara za kimataifa yameleteza utitiri wa makampuni. Karibia kila biashara kubwa au ya kati kwa sasa hufanywa na makampuni. Baadhi ya ndani na mengine ya nje.
Hatua hii njema kwa kiasi fulani imeongeza ajira japo ajira zenyewe hazina vigezo vya kuitwa ajira. Yatosha ziitwe kazi tu. Ajira hizi ambazo nyingi ni za umanamba zimekuwa zikifanywa na wazawa. Upande mmoja zimekuwa neema na upande mwingine zimekuwa laana.
Ni neema kwakuwa baadhi wanaweza kuishi japo kwa pato la mlo tu na kusiwe na akiba yoyote lakini pia zimekuwa laana kwakuwa ukihadithiwa baadhi ya mambo yanayoendelea huko waweza toa chozi.
Sio pote ila yapo maeneo yaliyoshindikana kama viwandani, migodini, miradi ya barabara na kwingineko waliko wawekezaji hasa wa kigeni. Hili ndilo limenituma kuandaa makala haya ili basi wenye fursa wasome na waelewe na wenye kutaka msaada waweza kuwasiliana nami na kuona la kufanya.
Nianze hivi, kampuni kwa mujibu wa sheria ni mtu( legal person). Kuna tofauti kubwa kati ya kampuni na mmiliki wake. Kisheria kampuni ikifanya kosa yatakiwa ishitakiwe kampuni na sio wamiliki au mfanyakazi kama mameneja, mkurugenzi n.k.
Nimewaona wengi hasa vijana ambao huyadai makampuni haki zao hufungua kesi wakiwashitaki wamiliki au mabosi wao. Hili ni kosa kubwa na wengi wao huwa wanashindwa zile kesi na badala yake kuanza kulalamikia mfumo wa nchi , mahakama au viongozi na hata chama tawala.
Ndugu hili halikusaidii. Hili sio la serikali wala rais wala nani ni suala ka kisheria. Kampuni yako imekukosea unataka kudai fidia umemshtaki mmilki au viongozi badala ya kampuni, ni lazima utashindwa kesi usimtafute mchawi wala kulalama kwa tuhuma za rushwa. Unapokosea taratibu sheria haina huruma inakata. Upo msemo usemao ( A law is a merciless sword) yaani sheria ni upanga usio na huruma unamkata yeyote anayeuchezea. Kampuni kama kampuni inao uwezo wa kushtaki kwa jina lake na kushtakiwa kwa jina lake,namna gani tutaona hapo chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...