Na   Bashir  Yakub.
Suala  la matunzo  ya  watoto/mtoto  lim ekuwa  ni suala  ambalo  wasomaji  wengi  wamekuwa  wakiniuliza sana. Wengi  wao  wanaouliza  ni  wale  ambao  wamezaa  nje  ya  ndoa  na  hivyo  kuna  utata  wa  matunzo  ya  watoto  na  wale  ambao  wamekuwa wana ndoa  lakini  sasa  tayari  wametengana  aidha  kwa  talaka  au  bila  talaka.  Niseme  tu kwa  ufupi  kuwa  suala  la  matunzo  ya watoto  linajumuisha  mambo  mengi  nami  nitaeleza  baadhi  tu.

1.HUWEZI  KUMLAZIMISHA  MTOA  MATUNZO  KUTOA  AMBACHO  HANA.
Kumekuwepo  na  tabia  ya  wazazi  hasa  upande  wa   wazazi  wa  kike   kuwalazimisha  wanaume  ambao  wamezaa  nao  na  kutengana  nao  kutoa  matunzo  ya  watoto  kwa  kiwango  cha  juu  kabisa  ambacho  pengine   kinazidi  hata  kipato  cha   mtoaji. Hili  si  sawa.  Ni  kweli sheria  inamlazimisha  mwanaume  kutoa  matunzo  ya  mtoto    lakini  haimlazimishi  kutoa  kuliko  anachopata. Sheria   haiseme  kwakuwa  mwanamke  anaishi  na  mtoto  wa  mtu  basi mwanaume   ndio  sasa afanywe  kitega  uchumi.  Inafikia  hatua  mwanamke  hafanyi  kazi  yoyote  isipokuwa  anategemea  ile  pesa  ya matunzo  ya  mtoto  ndio  iwe  kila  kitu  katika  maisha  yake.
Hii  ndio  sababu  hata  akipewa  kiasi   kinachotosha  haoni  kama  kinatosha  kwakuwa kinakuwa  na  njia  nyingi  kama  saluni, nguo za kuvaa,  pesa  ya  upatu, michango  ya  harusi  na  kitchen  party  na  kila  kitu  kinachohusu  maisha  yake binafsi.  Ieleweke  wazi  kuwa  kwa  mujibu  wa  sheria  pesa  ya  matunzo  ya  mtoto  haihusiki  na  haya.  Pesa  ya  matunzo  ya  mtoto  ni  pesa  ya  matunzo   ya  mtoto  kama   neno  lenyewe  lilivyo  na  linavyojieleza si  vinginevyo.

2.INARUHUSIWA  KUKATAA  IKIWA  UNALAZIMISHWA  KUTOA  MATUNZO YANAYOZIDI  UWEZO WAKO.
Ikiwa  mwanaume  analazimishwa  kutoa  kuliko  kipato  chake  basi  anaruhusiwa  kukataa  hata  kama  amri  hiyo  imetolewa  na  mahakama. Wengine  huandikishana  polisi  lakini  bado  haibadili  maana  kwakuwa  mtu  anatakiwa  kutoa  kulingana  na  uwezo wake  au  kipato  chake. Wapo  wazazi  hasa  wa kike   ambao  huwalazimisha  wanaume  kutoa  matunzo ya  kuwasomesha  watoto   international  schools  wakati  kipato  cha  mwanume  ni  shule  ya  kata. Sheria  inachokataza  ni  kukataa  kabisa   kutoa matunzo  ya  mtoto  lakini  haimlazimishi  mtu  kutoa  kilichomzidi.  Au  wengine  hulazimisha  kuwekewa  mpaka  wafanykazi  wa  ndani( house girl)  wakati  kipato  cha  mwanaume   hakiruhusu  jambo  hilo.

Huu  nao  ni  unayanyasaji  kwa  upande  wa  wanaume  na  haukubaliwi  na  sheria.  La  msingi  ni   kuwa  iwapo  utalazimishwa  kutoa  kuliko  uwezo  wako   we  kataa.  Na  kama  uamuzi  huo  umetolewa  na  mahakama  basi kataa  kwa  kukata  rufaa  kupinga  kabisa  jambo  hilo. Sheria  inaposema  matunzo  ya  watoto  haisemi  kuwa  watu  watoe  kuliko uwezo  wao  hapana. Sheria  ni  haki   na  haki  huzingatia  ukweli  na  hali  halisi  ya  jambo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...