Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Huawei,Ken Hu akizungumza katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita,uliokuwa ukijadili teknolojia ya simu za mkononi (5G).
Kizazi cha tano cha teknolojia ya simu za mkononi (5G) kinategemewa kuwa nguzo muhimu sana ya miundo mbinu katika ulimwengu ujao wa teknolojia. Hayo yamesemwa na Bwana Ken Hu, Makamu mwenyekiti wa Kampuni ya Huawei ambaye kwa kupokezana yeye ndiye Mkurugenzi Mtendaji kwa sasa.

Akizungumza katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita, Mr, Hu alisisitiza kwamba maono ya kuwa na teknolojia ya 5G yatafanikiwa kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali, ubunifu makini katika teknolojia na mageuzi katika mikakati ya kibiashara.

“Msukumo mkubwa wa kuwa na teknolojia ya 5G unahusisha mahitaji ya kumwezesha mtumiaji kupata urahisi kutumia, uwezekano wa vifaa vingi zaidi kutumia Internet katika maisha ya kila siku, na mahitaji ya kuwa na watoa huduma wanaozingatia sekta maalum pekee katika mapinduzi ya viwanda siku zijazo” Alisema Bwana Hu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...