Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kaimu Muuguzi Mkuu wa serikali Dkt. Amalberga Kasangala mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach kufungua rasmi “The Scientific Conference for Lugina Africa Midwives Research Network-LAMRN” tarehe 11.3.2015. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Ndugu Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa Kwanza wa “Lugina Africa Midwives Research Network” wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi kwenye meza kuu wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi tuzo Maalum kwa Bwana Maximillan Lugina, iliyotolewa na wajumbe wa mkutano wa “Lugina Africa Midwives Research Network” kwa ajili ya kumuenzi muasisi wa mtandao huo marehemu Profesa Helen Lugina ambaye ni mkewe. Profesa Helen alikuwa ni Muuguzi kutoka Tanzania aliyeasisi mkutano wa kwanza wa mtandao huo hapa nchini mwaka 1992.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa kwanza wa “Lugina Africa Midwives Research Network” uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach hapa Dr es Salaam tarehe 11.3.2015.
Wawakilishi mbalimbali kutoka nchi za Africa wanaohudhuria mkutano wa kwanza wa “Lugina Africa Midwives Research Network” wakimzawadia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mgolole mara baada ya kufungua rasmi mkutano huo huko Kunduchi Beach Hotel tarehe 11.3.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...