Mkurugenzi wa kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman (kulia) akihutubia wakati uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Bagamoyo, Pwani leo. Wengine kutoka kushoto ni, Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya, Mwenyekiti wa Riadha Tanzania Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende na Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo akisoma hotuba ya mheshimiwa waziri.
Kaimu Ofisa Michezo Wilaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon yanaandaliwa na kampuni ya 4Beli ya jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti chama cha Riadha Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende (wa pili kushoto) akizungumzia maendeleo ya riadha katika mkoa huo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon mjini Bagamoyo, Pwani leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...