Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.
………………………………………………………………………………..
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili
nchini.
nchini.
“Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama ishara ya kutakiana amani, upendo na mshikamano na tutaiombea nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu’’alisema Msama.
Msama aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’.Aliongeza kuwa ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...