Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na
vijana uliotolewa kwenye Kata zote za Manispaa hiyo, Victoria
Mboweto alipotembelea mradi wake wa duka la nguo, Kigogo
Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha
shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na
vijana katika Kata zake.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na
vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita
ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni
alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi.
Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya
kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Wapili
kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa
Jamii na Vijana wa Manispaa hiyo, Mwajuma Magwiza.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na
vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita
ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni
alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi.
Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya
kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Kushoto
ni mmoja wa wateja wa mwanamama huyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
(kushoto) akikagua mradi wa kuchakata vikoi na mashuka wa mmoja wa
wanufaika wa fedha za mkopo za akinamama na vijana wa Manispaa
hiyo, Thresia Mazwazwa (kulia kwake) alipotembelea mradi wake,
Sinza, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Manispaa hiyo imetenga
kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina
mama na vijana katika Kata zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...