Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Wataalam wa Mazingira
wameagizwa kutoa elimu ya mazingira kwa wawekezaji wa Mgodi wa Dhahabu wa
Sunshine uliyopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya .Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,
Injinia Binilith Mahenge jana alipotembelea machimbo ya Mgodi huo nakubaini kuwa
unaendeshwa bila kuzingatia Kanuni za Mazingira.
Katika ziara hiyo Mh. Mahenge alibaini kuwa mgodi huo hauna mtambo wa
kutibu maji-taka yake kabla ya kuyatiririsha katika mazingira pia bwawa linalotumika
kuhifadhi maji-taka hayo halikidhi viwango vya Kanuni za Mazingira pamoja na
kuzibwa kwa mfereji wa asili hivyo kuzuia mkondo wa mvua.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mahenge alitoa siku 30 kwa wataalam wake
kuwapatia elimu ya Kanuni za Mazingira wawekezaji wa Mgodi wa Sunshine ikiwa ni
pamoja na kuwataka wawekezaji hao kutekeleza kanuni hizo ndani ya siku 30 kuanzia
jana.
Wakati huo huo Mh. Mahenge alitembelea Machimbo ya Dhaabu ya Mek na
Mgodi wa Shanta Wilayani Chunya ambapo Wataalam wake Mazingira walibainisha
kuwa wawekezaji wa migodi hiyo wametiza kanuni za mazingira.
Sanjari na hayo Injiania Mahenge alikutana na Watendaji wa Halmashauri ya
Chunya na kukabidhiwa Mapendekezo ya Mradi Maalumu wa kulinusuru Ziwa Rukwa
ili lisitoweke kutokana na kilimo holela, uchimbaji wa madini na utirirshwaji wa maji-
taka kwenye vyanzo vya Ziwa hilo.
Katika makabidhiano ya Mapendekezo hayo Mh. Mahenge aliwaahidi
Watendaji wa Halmashauri ya Chunya kuwa atayafanyia kazi Mapendekezo yao lakini
pia aliwaomba na wao kuishauri Wilaya waingize Mazingira katika bajeti zao .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Binilith Mahenge akisiliza jambo kutoka kwa Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro kabla ya kuanza Ziara yake ya siku mbili Mkoani humo jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge (katikati), wakijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mh. Deodatus Kinawito (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde (kulia) wakati wa Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani humo jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Machimbo ya Dhahabu katika Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya, Bwana Andy Wu (kulia), katika ziara ya Mazingira Mgodini humo jana na wakati katika picha ni Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge, akionesha Bwawa linalotumika kuhifadhi Maji-taka yenye Sumu kutoka kwenye Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya jana, huku akiwataka Wawekezaji wa Mgodi huo kuboresha Bwawa hilo ili kukidhi Kanuni za Mazingira za Tanzania . (Picha na OMR)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...