Na John Gagarini, Chalinze

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara yake kwenye Jimbo hilo ambapo ameendelea kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mbali ya kuangalia masuala ya maendeleo pia kwenye suala la michezo hakuwa nyuma kwa kuweza kukabidhi jezi kwa kijiji cha Mboga ili kuendeleza michezo kwa vijana walioko kwenye kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,Mh. Ridhiwani Kikwete  akimvalisha kofia ngumu ya pipikipiki kama ishara ya kumkabidhi mwenyekiti wa Wastaarabu Camp,Bi. Elizabeth John wa tawi la Wastaarabu Camp huko Kijiji cha Mboga wilayani Bagamoyo.
Mwenyekiti wa tawi la Wastaarabu akizungumza huku akiwa amekaa kwenye pikpiki aliyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete alipotembelea Kijiji cha Mboga kata ya Msoga.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi jezi diwani wa kata ya Msoga,Mohamed Mzimba kwa ajili ya mashindano ya kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi jezi moja ya viongozi wa timu ya Mboga,Rashid Adam kwa lengo la kuhamasisha michezo kwenye kata ya Msoga .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...