Na John Gagarini,Globu ya Jamii - Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete jana alianza ziara kwenye Jimbo hilo ambapo ametembelea shughuli mbalimbali pamoja na kujua changamoto zilizopo kwenye Jimbo lake.
Ridhiwani alitembelea kata ya Pera na kuzungumza na wakazi wa vitongoji mbalimbali ambavyo vinaunda kata hiyo ambapo leo ametembelea kata ya Kibindu nako alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa vitongoji vilivyopo kwenye kata hiyo.
Mbunge huyo atakuwa na ziara ya wiki moja kutembelea kata mbalimbali za Jimbo hilo na kujionea shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule za msingi na sekondari, barabara, zahanati na kufanya mikutano ya hadhara ya wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kitongoji cha Malivundo wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na moja ya wanafunzi wa shule ya Msingi Malivundo wakati wa zaiara yake kutembelea shughuli za maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia matofali alipotembelea ujenzi wa shule ya Msingi wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...