Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemkabidhi gari aina ya Toyata
IST kwa Bwana Juma Said Alli mkazi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma
mara baada ya kuiba mshindi katika droo ya wiki ya pili ya promosheni
ya Airtel yatosha zaidi.
Zawadi hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni
15 ilikabidhiwa kwa Alli mwishoni mwa wiki na Meneja wa Airtel Kanda
ya Kati, Stephen Akyoo.
Akizungumza mbele ya vyombo vya habari wakati akikabidhiwa gari hiyo
aina ya IST, yenye namba za usajili T778 DCZ, Alli alisema shughuli
zake ni ukulima wa mazao mbalimbali katika Kijiji cha Ololimo na ana
mke mmoja na watoto wawili.
“Sikutegemea kushinda ingawa nimekuwa
nikijiunga mara kwa mara na kifurushi cha Yatosha, kila ninaponunua
vocha za Airtel na ninamshukuru Mungu nimeshinda kutokana na Yatosha
ya Shilingi 500 tu. Hivyo nawahimiza watanzania wenzangu wasikate
tamaa kwani na wao wanaweza kubahatika kama mimi na kujishindia gari
hili zuri,”alieleza Alli.
Kwa upande wake Meneja wa kanda ya kati bwana Stephen Akyoo alisema
"tunao washindi wengi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini
ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Mtwara, Mbeya,
Tanga,Mwanza,katavi na sasa Dodoma.
Promosheni hii bado inandelea ni
rahisi sana kwa kutumia vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au
mwenzi moja kwa moja unaunganishwa kwenye droo ya Airtel yatosha na
kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST kila siku.
Vifurushi vya
Airtel yatosha vinapatikana kwa kupiga *149*99# , au kwa kununua vocha
ya Airtel yatosha au kununua kupitia Airtel Money kwa matumizi yako ya
kawaida kabisa unapata nafasi ya kujishindia gari "
Wakati huo huo Airtel imetangaza washindi saba wa wiki ya nne ya
promosheni ya Airtel yatosha waliopatikana kupitia droo iliyofanyika
siku ya ijumaa katika makao makuu ya Airtel Moroco, washindi hao ni
pamoja na Juma Mapande (30) mkazi wa Pwani, Eusedio Onesmo
Kipalile(48) mkazi wa Njombe, Suleiman Daudi Onesmo (20) Mkazi wa
Mwanza, Seleman Kikondi Kimu (29) Mkazi wa Morogoro, Hassan Saidi
Kimbe(28) Mkazi wa Dar es Saalam, Mohamed Ahmed Hamis (47) mkazi wa
Manyara pamoja na Aivan Mbogambi Saigwa (35) Mkazi wa Dodoma
Washindi hawa watakabithiwa magari yao wiki hii pindi taratibu zote
za makabithiano zikikamilika
Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto) akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto) akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
Mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 778 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...