Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Hizi ndizo nyumba zinaeleweka na zinazotakiwa kuhamasishwa ili wataanzania wote tuwe na makazi bora.
ReplyDelete