Tokyo,Japan. Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi Machi 21,2015 ambapo wanamuziki wa Eagle's Vission watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super Nyamwela.

Katika onyesho hilo wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan,Fresh Jumbe Mkuu na Abbu Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa Sehemu inaitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.

Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali kwa ujumla,Pia uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa. Wadau msikose kujitokeza kwa wingi katika Onyesho hili waswahili usema 'Chereko Chereko na mwenye mwana"
Fresh Jumbe akifanya yake katika moja ya shoo zake huko Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...