Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu (pichano) mapema leo hii ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Jimbo la Kigoma Kasikani,Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema.
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.

Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

CHANZO: EATV.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. DON'T WORRY MR. ZITTO KABWE YOU WILL BE FINE, JUST JOIN A DIFFERENT PARTY AND RUN FOR MP AGAIN AND YOU WILL CONSEQUENTLY WIN THE SIT AGAIN, WE RECOGNISE YOUR JOB AND WE GOT YOUR BACK WE WILL NOT DUMP YOU.

    ReplyDelete
  2. Chadema roho mbaya zenu ndio zinawaponza kukivuruga chama chenu

    ReplyDelete
  3. Pole sasa kaka zito, hayo ni majaribu tuu, ukweli ni kwamba yaliyokukuta yanatokana na kazi yako nzuri ya kuwazindua watanzania nini kinaendelea ktk mali zao na ukuwaji wa uchumi. Huwezi kuwa mwema kwa wote hata hao chadema inaonekana nao ni mafisadi ndio maana wakakutafutia zengwe wakudondoshe usiwahi kufichua udhaifu wao. Tuko pamoja kaka na mungu atakupa nguvu na lenye kheri nawe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...