Tayari maandalizi ya ule mpango wa kujenga barabara ya njia sita (tatu kila upande) Dar es Salaam – Chalinze-Morogoro (km 200) Express Way umeiva ambapo awamu ya kwanza itahusisha barabara ya Dar es Salaam (Biti Titi Jnct) – Chalinze (km 100) Express Way kwa utaratibu wa Public Private. 
Barabara hiyo mbadala ambayo itakuwa ni ya kulipia itajengwa kwa njia sita (6 lanes). 

Barabara iliyopo sasa itaendelea kutoa huduma kwa wale ambao hawako tayari kutumia barabara ya kulipia. Habari njema ni kuwa, Wahandisi washauri wa michoro ya barabara hiyo tayari wameonyesha jinsi njia sita zitakavyojengwa. Kazi hii inategemewa kuanza mwaka huu, kwa mujibu wa wataalamu hao walipokuwa wakiwakilisha ripoti ya utafiti wa awali wa michoro ya barabara hiyo, New Afrika Hotel. Barabara hii itajengwa kwa kwa utaratibu wa ubia kati ya serikali na makampuni binafsi (Public Private Partnership -PPP).
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar - Chalinze uliofanyika jijini Dar es salaam.
Jopo la Wataalamu washauri katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara  ya Dar - Chalinze.
Ramani ya barabara ya njia sita (tatu kila upande) ya Dar es Salaam - Chalinze - Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu, mm nishakinai na hizo Ramani bira ya action....tuanzie kigamboni city imeshajengwa kwa ndimi.....bonde la msimbazi park iko wapi?....bandari kubwa na ya kisasa huko bagamoyo iwapi?....acheni kuchezea akili za watanzania mtakavyo....na hakuna kitu kinachonikera kama hiyo bara bara utasikia eti itakamilika baada ya miaka 5 au 6 hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi....ndugu zangu watanzania mm huku niliko kitu muhimu kama hicho watu wanapiga kazi masaa 24 na baada ya miezi 2 au 3 kitu na box...lakini hapo bongo kwenye mambo ya maana mwendo wa kinyonga.

    ReplyDelete
  2. Du programu kibao,hizo njia sita ni za kufikirika vichwani tu,tumechoka na maneno yenu!

    ReplyDelete
  3. duuh mafoleni ya kimara, mbezi, kibamba, mlandizi yanarudi tena!! kwann walipofikiria mabasi yaendayo kasi wasingemalozia na hili kabisa?? hio ndo bongo daslama.

    ReplyDelete
  4. Barabara ya njia sita kuanzia bibi titi / morogoro road... sasa ile ya mabasi yaendayo kwa kasi ambayo tayari imejengwa mpaka kimara inavunjwa au inakuwaje?

    ReplyDelete
  5. Je, kutakuwa na uwiano baina ya lanes ana spidi kali = ajali zaidi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...