Dr. Natalius Kapilima wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu
Bw. Exadius Nthono wa Lesotho katika mkutano wa mwaka wa wahasibu waandamizi
unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere ambapo NHIF inatoa
huduma za upimaji afya bure.
Na Catherine Kameka
WADAU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wameuomba Mfuko huo
kuendeleza programu za upimaji wa afya bure ili kuwasaidia wanachama
wake na wananchi kwa ujumla kujua hali za afya zao lakini pia kuepekana
na maradhi yasiyoambukiza.
Hayo wameyasema Dar es Salaam jana katika mkutano wa Wahasibu
Waandamizi wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, unaofanyika
katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere ambapo NHIF ilishiriki
kwa kuwa na banda la elimu kwa umma na upimaji wa afya bure
uliokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya namna ya kujikinga na
maradhi yasiyoambukiza kama moyo na mengine.
Pamoja na ombi hilo, NHIF imekuwa ikiendesha upimaji katika maeneo
mbalimbali ya nchi kwa lengo la kuwasaidia wananchi kufahamu afya zao
lakini pia kuwapa ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi hayo ambayo
yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na matibabu yake ni ya ghari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...