Katika mwendelezo wa kuwa karibu na wateja wake benki ya NMB imezindua mtandao utakaowaunganisha wateja wake wakubwa ‘Executive Network’ kwa jiji la mbeya ikiwa na lengo la kuwafanya kufurahia zaidi huduma za kibenki kutoka NMB.
Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya na kuwakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka vitongoji mbali mbali ikiwemo Kyela, Mbozi,Tunduma, Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe waliopata fursa ya kuwa kwenye mtandao wa wafanya bishara wa NMB.
Mtandao huu unaounganisha wateja wakubwa wa NMB vile vile umezinduliwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo; Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya ikiwa ya nne.
Maafisa wa NMB wakifurahi pamoja na
mteja wao baada ya uzinduzi rassmi wa mtandao wa ‘NMB Executive Network’
Sehemu ya wateja wakubwa wa NMB walioalikwa
katika uzinduzi huo.
Mmoja wa
wateja wakubwa wa NMB akiomba ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo na benki
hiyo wakati wa hafla iliyowakutanisha
wateja wakubwa wa benki ya NMB.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa NMB, Masato
Wasira(kushoto) na Mtaalam Mwandamizi wa bidhaa za hazina kwa wateja wakubwa ,Ronald
Kato wakiwa pamoja na wateja wa NMB
kutoka kampuni ya Sunshine Mining ya Chunya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...