Benki ya NMB imeendela kuwapiga msasa wateja wake wa mtandao wa NMB Business Club Wilaya ya Ilala kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao, fedha za kigeni, bidhaa na huduma zitolewazo na benki ili kuwawezesha kuendelea kuwa vinara wa biashara.

Katika semina hiyo iliyowakutanisha wajasiriamali zaidi ya 300, iliwapa fursa vilevile wanachama wake kubadilishana mawazo na wenzao hasa katika ulimwengu wa biashara.
Kaimu mwenyekiti wa NMB Business Club Wilaya la Ilala-Dar es Salaam Bw. Chatele Eliakimu Sando akielezea jinsi wana NMB Business Club Wilaya ya Ilala walivyonufaika na klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na wanavyoendelea kufurahia huduma na bidhaa kutoka benki ya NMBAkitoa shukurani kwa niaba ya wanachama wake kwa uongozi wa benki ya NMB kwa kuandaa semina ambazo zinatoa mafunzo yanayowajenga wanachama wa NMB Business Club.
Afisa Bidhaa wa NMB-Chacha Borondo akielezea kuhusu bidhaa na huduma zitolewazo na NMB
Sehemu ya wanachama hao wakibadilishana mawazo.
Mhazini wa NMB Kanda ya Dar es Salaam kitengo cha Hazina, Joseph Funuguru akitoa mafunzo juu ya fedha za kigeni kwa wateja wa NMB walio katika mtandao wa NMB Business Club katika semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...