Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Rais, utaumia kwa kuwasaidia watu kila kukitokea mafuriko. Tafuteni suluhisho la haya matatizo ili matatizo kama haya yasijitokeze tena hapo baadaye. Wakaazi wa Dar, jitahidini kuimarisha usafi, uchafu nao unasababisha taka kuziba mifereji inayopitisha maji. Dar ni jiji kubwa la kibiashara na ni namba one kwa uchafu Tanzania kuliko majiji mengine.

    ReplyDelete
  2. Kweli Tanzania bado tunasumbiliwa na Umatumbi kwelikweli. Hivi Building codes haiwezekani kabisa kuzianzisha na kuzisimamia? Rais, anaona mwenyewe ubovu wa viwango wa ujenzi, na mahali pa kujenga lakini Sidhani kama atahakikisha nchi inakuwa na Building codes/standards. Hapo kashaweka "check mark" yake na inatosha. Please please wabunge tungeni codes na miji isimamie ili watu wajenge na miji ijengwe kwa kufuata viwango na mipango. SHAME SHAME SHAME.

    ReplyDelete
  3. Mdau namba mbili nakupa kudos!

    ReplyDelete
  4. Building codes zipo. Sheria zinazozingatia good city planning zipo. Kile ambacho hakuna ni kwamba HAKUNA UTEKELEZAJI. Na hili tatizo lipo katika kila sekta nchini Tanzania. .................. Mfano, sheria za barabarani zipo lakini ni sheria za porini zinatumika Tanzania. ........ Fikiria sekta nyingine yeyote na utaona matatizo ni yale yale. It is sad.

    ReplyDelete
  5. Ninyi wakaaji wa Dar, tunzeni Jiji lenu, kama wanavijiji wanavyotunza vijiji vya. Msitegemee serikali iwafanyie kila kitu!

    Rudisheni utaratibu wa Nyumba Kumi. Kila nyumba ishiriki katika kuzibua mirao ya maji na kusafisha kila taka na mchanga uliomo mitaroni.

    Hii ni mvua tu; tsunami ikija...Dar kwisha.

    ReplyDelete
  6. Acheni uvivu na ujinga wa kusign mikataba ya fly over za tazara....just tengeneza drainage system na fix building codes too much ujinga kama hatuna wasomi..amboa wapo ila hawapewi ajira...lini tutajiajiri na kujiamini....

    ReplyDelete
  7. The mdudu, yaani buguruni iko vile vile? Sasa nikuulizeni nyie wote mnaochongachonga kuhusu sisi wa ugaibuni....(1) hivi hiyo buguruni KUNA MBUNGE, mkuu wa wiraya, mkuu wa mkoa, na meya? Nakuombeni sn mnipe Jibu la ndio au hapana kisha tuchonge vizuri na mtanikoma hii haikubariki kabisa lazima tuogope dhambi mjomba Michozi nakuomba sn wamwagie huu UPUPU.

    ReplyDelete
  8. Wale waliosomea mipango miji wanafanya nini hata watu wanajenga kiolela. Maeneo mengine ukienda utashangaa hapa mtu anapiga mswaki, hapa sebule njia ya kuingilia hakuna kila nyumba imeangalia kivyake. Mitaro ndiyo maana kukinyesha kidogo mafuriko hayo.

    ReplyDelete
  9. We kweli mdudu tena wa chooni.kujiona upo nje ya nchi ndo ulete dharau? Nani akukome,kuandika kwenyewe hujui daily ktk herufi L unaweka R . Be positive ktk hoja onesha njia mbadala.si majigambo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...