Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.
Mashaallah! Mwenyeezi Mungu amuongezee kila la kheri Mzee S.S.Bakhresa kwa kutoa ajira kwa watanzania wengi. Ni aghalabu hapa duniani kukuta mtu wa namna yake. Tajiri asiyejitangaza. Nina hakika ni wengi wetu tulikuwa tukimsikia tu bila kujua anafananaje. Naomba wenye vipato vyao waige mfano wa huyu baba. Mungu akubariki baba.
ReplyDeleteHONGERA SANA S.S.BAKHESA kwa kuamua na kukubali ushauri mzuri bila shaka wa wataalamu wa ndani na nje katika kubuni bidhaa mbalimbali 'product diversity' kukidhi walaji mbalimbali wa ndani na nje pia.Huduma na bidhaa zisizo kifani kwetu sote.Rais amepata bahati kubwa kufungua uwanja mzuri kule Chamazi na leo anafungua tena wonderful studios hapa Tabata.Watanzania tuone fursa hizi hapa nyumbani, wakusoma junalism, marketing n.k wafanye vizuri zaidi ili kupata ajira ili wawe wadau wakubwa katika tasnia hii.hongera SSB.
ReplyDeleteMzee S.S,Bakheresa mwenyezi mungu amuongezee ,ni tajiri asiye penda makuu wala kujitangaza na kuuza sura,mwekezaji mzalendo anayezalisha ajira kwa wengi,apendi kujiingiza katika siasa
ReplyDelete