Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Mgahawa wa Samaki Samaki umeanzisha mpango wa kuchangia Elimu kwa watoto yatima kwa kila mtu atakayekula katika migahawa ya samaki samaki itatolewa sh.1000 kwa bei halisi na sio kukatwa mteja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,Afisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki,Edward Lusala amesema Samaki Samaki imefikisha miaka nane tangu kuanza kwake na wameona kuna umuhimu wa kuchangia katika kundi la watoto yatima.

Amesema kuwa wanawafundisha ufundi watoto yatima ili kuweza kufikia hatua ya kujiajiri wenyewe katika sekta uchongaji wa vinyago pamoja na mitumbwi.

Lusala amesema kundi la watoto yatima linahitaji kuangaliwa kwa karibu ili kuweza kufikia malengo yao kwa kuwasaidia katika sekta mbalimbali.
Afisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki,Edward Lusala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, juu ya kuchangia sh.1000 kwa kila mtu ambaye atakula chakula katika migahawa ya Samaki Samaki na fedha hiyo itatumika kwa kusaidia Elimu kwa watoto yatima.Kulia ni Meneja Masoko wa Samaki Samaki,Njama Matumbo na kushoto ni Meneaja Mauzo wa Coca Cola Kwanza Dar es Salaam,Ruqaiya Alibhai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nani kala chipsi na samaki wote?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...