.jpg)
1.0 MISWADA
YA SHERIA:
1.1
MISWADA
YA SHERIA YA SERIKALI:
a) Kusomwa
kwa mara ya Kwanza na hatua zake zote:
Katika Mkutano huo, Kwa mujibu wa Kanuni
ya 93(3) ya Kanuni za Bunge Toleo la Aprili 2013 Jumla ya Miswada Sita (6) itawasilishwa
Bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote. Miswada hiyo
ni:
(i)
Muswada wa Sheria ya kupata habari wa Mwaka 2015(The Access to Information Bill, 2015),
(ii)
Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015 (The Media Services Bill, 2015),
(iii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 [The Fair Competitio (Amendment) Bill,
2015],
(iv)
Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa Mwaka, 2015(The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015),
(v)
Muswada
wa Sheria ya Miamala ya Kiektoniki wa Mwaka 2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015),
(vi)
Muswada
wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The
Natural Gas Bill, 2015).
b) Kusomwa
kwa mara ya Pili na hatua zake zote:
Aidha, Jumla
ya Miswada 15 itasomwa kwa mara ya Pili Bungeni na kupitishwa na Bunge katika hatua
zake zote kwa mujibu wa Kanuni ya 86(1) ya Kanuni za Bunge. Miswada hiyo ni:
(i)
Muswada
wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non- Citizens Employment Regulation Bill, 2014];
(ii)
Muswada
wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa
wa Mwaka 2015 [The National
Payment Systems Bill, 2015],
(iii)
Muswada
wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 (The Tax Administration Bill, 2014.
(iv)
Muswada
wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014 (The
Statistics Bill, 2014),
(v)
Muswada
wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014],
(vi)
Muswada
wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa
Mwaka 2014 [The Disaster
Management Bill, 2014],
(vii)
Muswada
wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill,
2014],
(viii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Wharehouse Receipts (Amendment) Bill,
2014],
(ix)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014],
(x)
Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa
Mwaka 2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014],
(xi)
Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014],
(xii)
Muswada
wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill,
2014],
(xiii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous
Amendements) (No. 2) Bill, 2014] ,
(xiv) Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka
2014 [The Budget Bill, 2014], na
(xv)
Muswada
wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa Mwaka 2015 [The Youth Council of Tanzania Bill, 2015],
1.2
MUSWADA
BINAFSI WA MBUNGE:
kwa Mujibu wa kanuni ya 81 (1) ya
Kanuni za Bunge, katika Mkutano ujao wa 19 kunatarajiwa kuwasilishwa
Muswada Mmoja wa Mbunge Binafisi ambao ni Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana
la Taifa wa Mwaka 2013 (The Nationa Youth
Council Bill, 2013) wa Mheshimiwa John John Mnyika. Muswada huu utasomwa
kwa mara pili na hatua zake zote.
2.0 MAAZIMIO
NA ITIFAKI MBALIMBALI
Pamoja
na Miswada hiyo, katika Mkutano wa 19, Bunge linatarajia pia kuazimia Maazimio Mawili
kama ifuatavyo:
1.
Azimio la kuridhia Mkataba wa Msingi na
Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika.
2.
Azimio la kuridhia Makubaliano ya Msingi
ya Ushirikiano katika Bonde la mto Nile (Agreement
on the Nile river basin Co-operative Framework- CFA).
3.0 MASWALI:
Aidha, katika
Mkutano huu wa 19 wa Bunge, Jumla ya
Maswali ya kawaida 170 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa ambapo ni wastani wa
Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku za Alhamisi.
Aidha kutakuwa
na kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kwa Mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ambapo jumla
ya Maswali 18 ya msingi yataulizwa na
kujibiwa na Mhe. Waziri Mkuu.
Ratiba Kamaili
ya Mkutano wa Kumi na Tisa (19) na jinsi shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa
baada ya Kamati ya Uongozi kukutana Jumatatu tarehe 16 Machi, 2015 ambapo
itatolewa na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz
Imetolewa na:
Idara ya
Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi Ndogo za
Bunge
DAR ES SALAAM
13 Machi, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...