1Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akizungumza mapema leo
katika siku ya kwanza ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba
yanayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma. Kutoka kulia
ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas
Kandoro, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw.
Jumanne A. Sagini na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Bw. Zuberi Samataba.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini akitoa mada kuhusu kazi na majukumu ya Wakuu wa Wilaya katika semina hiyo iliyoanza leo tarehe 16 hadi 19 Machi 2015.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja, ambaye pia ndiye
mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea
mjini Dodoma. UONGOZI Institute ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais
inayoshughulikia mafunzo kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na kufanya
utafiti na ushauri wa sera kwa serikali.
Mshiriki
wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Shaban Kissu akichangia mada
wakati wa mafunzo. Mada moja wapo zilizojadiliwa leo ni kuhusu mahusiano na
mawasiliano baina ya serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa.
![]() |
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda akizungumzia kuhusu changamoto
mbali mbali za Wakuu wa Wilaya. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na maadili na
sheria za kazi.
|
Baadhi ya wahudhuriaji wa kundi la Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba wakifuatilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mafunzo ya Wakuu wa Wilaya Wapya yanayoendelea mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...