Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza
na wageni waliofika ofisini kwake kumjulisha kuhusu Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni
lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania na kuhusisha nchi 18
tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, wakwanza kulia ni Bw. Ramadhani Madabida na anayefuata ni
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
Bw. Ramadhani Madabida (kulia) akifafanua jambo walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakwanza kushoto kumpa taarifa ya Tamasha
la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika
nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha nchi 18. katikati ni Rais wa Kilimanjaro
Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz (wapili kulia) akielezea jinsi walivyojiandaa
kufanikisha Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalohusisha nchi 18 walipokutana na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto). Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na kulia
ni Bw. Ramadhani Madabida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...