Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Jimbo la Singida, Martha Mlata (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dkt. Miganda Manyahi (kulia), jijini Arusha kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inafanya ziara katika miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kujionea hatua ya utekelezwaji wake pamoja na kuzungumza na watendaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda (kulia) mara baada ya Kamati hiyo kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya kupokea taarifa ya mkoa kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kushoto) akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye chumba cha kuendesha mitambo ya umeme ( control room) ndani ya kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha.
Meneja Mradi katika Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha KIA Mhandisi Emmanuel Manirabona (kulia) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo hicho kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...