Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa huduma ya treni ya abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne Machi 24, 2015 kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam saa 11 jioni.
Wananchi wanaotaka kusafiri wafike stesheni zilizo karibu yao kwa ajili ya kukata tiketi ya safari hiyo.
Huduma ya usafiri wa reli ilisitishwa wiki mbili zilizopita Machi 6, 2015 baada ya eneo la tuta la reli kati ya Stesheni za Kilosa na Kidete kukuharibiwa vibaya na mafuriko kulikosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha sehemu hizo.
Kazi ya ukarabati wa eneo hilo iliyokuwa ikifanywa usiku na mchana na Wahandisi na Mafundi wa TRL ilikamilika siku ya Jumanne usiku Machi 17, 2015.
Halikadhalika muda wa kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya Dar kwenda Kigoma na Mwanza utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar katika siku za Alhamis na Jumapili ni saa 11 jioni kutokea Kigoma na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo A. Kisamfu
Dar es Salaam
Machi 20, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...