Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi  sasa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.

Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao ndiyo itakayoamua huduma hiyo ya usafiri wa treni za abiria  itarejea lini.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya kwa niaba ya 
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu 
Mkurugenzi Mtendaji –TRL
Dar es Salaam
Machi 06, 2015 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, mm naona huyo mkurugenzi kazi imemshinda kila mwaka hilo tatizo kwao ni lazima na bado yupo kazini. ..ndugu zangu watanzania ogopeni sn watu kama hao wasio wabunifu hao wapo kwa ajiri ya mishahara yao tu na wala sio kuleta ubunifu endelevu. ..huku niliko kitu kama hicho kikitokea na siku hiyo hiyo kazi hana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...