Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akiwa na ujumbe wa Kampuni ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore ofisini kwake. Kampuni hiyo imeingia mkataba na Tanzania katika uandaaji wa mpango kabambe (Master plan) wa Jiji la Arusha.
Katibu mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akifafanua jambo katika kikao kifupi ofisini kwake, baina ya Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willium Lukuvi, National Housing Coorporation na ujumbe wa Kampuni ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akipokea zawadi ya picha, ambayo alipigwa alipokuwa ziarani Singapore, anayemkabidhi ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Surbana International Pty Ltd,Pang Yee.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angela Kairuki akipokea zawadi ya picha ambayo alipigwa alipokuwa ziarani Singapore, anayemkabidhi ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Surbana International Pty Ltd,Pang Yee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Kairuki, hongera sana kwa kuonekana kuwa na heshima na busara kubwa na mfano wa kuigwa na wanawake wengine, wenye tabia ya kuiga kila kitu kutoka kwa wazungu, hata mavazi nayo wanaiga. Hongera saaana hata mavazi yako yanaonyesha wewe ni kiongozi. Wanawake wengine wakiona wazungu wamevaa suruali, naye anataka avae. Hivi sisi waafrika, hasa wabongo tutaacha lini haya mambo ya kuiga hata na vitu visivyoeleweka. Mwishowake tutaanza kuishi na mbwa ndani ya nyumba.

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono mchangiaji wa kwanza hapo. Kwa kweli hata mimi sijawahi kumuona huyu Mheshimiwa kuvaa vya ajabu ajabu. Keep it up mpendwa. Kina mama wengine ambao ni viongozi hebu basi tuige mfano huu mzuri. Mwingine ni Mheshimiwa Dr. Fenella Mkangala.Nawapenda sana

    ReplyDelete
  3. Kwanza kabisa ingawa hii ni nchi huru na una haki ya kutoa maoni yako kwa hili umechemsha.,huo utamaduni unaouzungumzia ni upi haswa?! Maana utamuduni wa Mwafrika ulikuwa ni kukaa uchi kabisaaaa....Kwenye suala la mavazi ni vizuri ukawaacha watu wavae wanavyotaka acha kuwanyapapa wanawake .,suruali ni moja ya vazi la heshima sana tu kama ilivyo kwa gauni na sketi so long as linafit vizuri (lisiwe dogo ama kubwa sana) na pili huyo huyo dada unayemsifia leo kavaa gauni naye huwa anavaa suruali sana tu, sasa sijui siku akivaa suruali utamvua uafrika wake na kumshutumu?!

    ReplyDelete
  4. Inaonekana mdau wa hapo juu punguza lawama na kunyoosha vidole kwa wenzio. Nahisi unatakiwa kuoma zaidi na kupunguza kuandika, mpaka hapo utakapopevuka kimaarifa!

    ReplyDelete
  5. Brenda dada yangu naona uko nyuma sana ya wakati. Unapozungumzia utamaduni wa mwafrika ulikuwa ni kukaa uchi, unajua ilikuwa mwaka gani? Hayo ni mambo ya kale kabisa wala hayakuwepo kwenye kizazi hiki. Katika kizazi hiki cha kwetu hatukuyakuta hayo unayoyasema. Ukweli ukizungumzwa ni vizuri tukubali, hata kama unauma. Katika kizazi chetu tunafahamu/ tumezaliwa tumekuta mwanamke akivaa gauni na sketi, vilvile mwanaume akivaa suruali.

    Mimi niko katika hiyo nchi yenye uhuru mkubwa wa kila kitu, ila ni mchanganyiko, hawakulazimishi kuwaiga wanavyofanya wao wanaita mchanganyiko wa tamaduni (multicultural). Huku hata akipita mwanamke wa kisomali utamtambua kwa mavazi yake, akipita kahaba vilevile utamtambua kwa mavazi yake, akipita shoga naye vilevile, na hulazimishwi kufuata wao wanavyotaka. Wakati wa summer utaona viroja.
    Hata huko bongo hakuna anayekulazimisha kuvaa vyovyote, ila nilichomuelewa huyu aliyeanzisha hii maada anataka kutukumbusha kuwa viongozi wetu wanatakiwa watuonyeshe mfano. Mavazi sidhani kama ni maendeleo, ukitaka tukuone unakwenda na wakati, zalisha ajira kwa wabongo, ili kupunguza ukata na kuleta maendeleo sio masuruali.

    Hili swala mavazi ya heshima kwa viongozi ni vizuri likaingizwa kwenye Tume ya Maadili ya Umma, badala ya kuwang'ang'ania akina vijisenti peke yao wawe wanaangalia na viongozi ambao wanaashiria tabia mbaya kutokana na mavazi yao.

    Vilevile maandiko matakatifu yanasema mwanaume asivae mavazi ya mwanamke, na mwanamke asivae mavazi ya mwanaume ni chukizo mbeleza MUNGU.

    Ndio maana kunapokuwa na michanganyo mingi kama hii basi nchi kama bongo kujitegemea inakuwa ni ndoto, tutaendelea kuomba misaada kila siku, mpaka tubalishe fikira na mitazamo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...