Ukuaji wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.
Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.

Wakati hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza kusomwa na wengi kitu ambacho kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao wamejipanga.
Watanzania hawanabudi kuwa makini sana na kuwa waangalifu sana wanapo takiwa kuingiza taarifa zao binafsi na wanapo takiwa kufata maelekezo wa kutekeleza miamala kupitia mitandao kwenye vyanzo vyenye utata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...