UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yote yenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 235.
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliono.
Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.
Ndugu Mfaume Kimario, Afisa Masoko na Uhusiaono Mwandamizi wa UTT AMIS akiwaelimisha baadhi ya wafanyakazi wa Teofili Kisanji University tawi la Tabora kuhusiana na faida za kuwekeza fedha zao kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inaendeshwa na UTT AMIS.
Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga aliyesimama kulia akiwaelimisha baadhi ya maofisa wa CRDB Tawi la Tabora kuhusiana na uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo Bwana Sdney Bakari. CRDB Bank ni mdau muhimu wa UTT AMIS kwanza ni muangalizi wa mali za wawekezaji kmifuko na pia ni wakala wa kutoa huduma za Mifuko ya uwekezaji inayoendeshwa na UTT AMIS.
Baadhi ya waendesha Bodaboda mjini Tabora wakipewa elimu ya uwekezaji na Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS Ndugu Mfaume Kimario. Kiwango cha chini cha kuwekeza ni 5000/= tu kwa Mfuko wa Umoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...