Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Godfrey Ngonyani
(kushoto) akimkabidhi zawadi mtarishaji wa kipindi maarufu cha Power Breakfast Bw. Phillip Mwihava
baada ya kumalizika kwa semina ambayo PSPF iliandaa maalum kwa watendaji kutoka Clouds Media.
Lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha kwanini PSPF inaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa waajiriwa
wapya hapa nchini. Anayeshuhudia Bibi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF.
Afisa uhusiano Mwandamizi wa Clouds Media Bw. Kelly Michael (kushoto) akisisitiza jambo wakati
wa semina iliyoandaliwa maalum kwa watendaji wa Clouds Media, kulia ni Said Mohamed maarufu
kama Bonge naye akifatilia kwa makini semina hiyo iliyolenga kuwaelimisha juu ya huduma na bidhaa
mbalimbali za PSPF.
Watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wageni wao kutoka Clouds Media wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya semina iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya watendaji wa Clouds Media.
Na Mwandishi Wetu
Mwanzoni mwa wiki hii wafanyakazi wa Clouds Media Group walipata fursa ya kutembelea Makao Makuu ya
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa lengo la kujengewa uwezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na PSPF.
Ziara hiyo iligawanyika katika sehemu mbili, ya kwanza ilikuwa ni semina na ya pili ilikuwa kutembelea maeneo
mbalimbali ya PSPF ili kuweze kujionea utendaji kazi wa Mfuko huo ambao kwa sasa ndio changuo la kwanza kwa
waajiriwa wapya nchini.
Semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bibi. Neema Muro ambaye aliwaeleza kwa kina
juu ya bidhaa na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Bibi. Muro alisema Mfuko wa PSPF una mafao ya muda mfupi ambayo ni fao la uzazi, mkopo wa elimu, fao la
kujitoa, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mkopo wa nyumba na mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu.
Aliyataja mafao ya muda mrefu kuwa ni fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao la mirathi na fao la kufukuzwa au
kuachishwa kazi.
Pia Mkurugenzi huyo alieleza kwamba PSPF ina mpango wa uchangiaji wa hiari ambao mwanachama wake ni mtu
yeyote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na anaweza kuwa katika sekta rasmi na hata katika sekta isiyo
rasmi, kima cha chini cha kuchangia nia shilingi 10,000 tu kwa mwezi. Mafao yanayotolewa chini ya mpango huu ni
pamoja na Fao la elimu, Fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kifo, fao la ugonjwa au ulemavu na fao la kujitoa.
Kwa upande wa uwekezaji, Bibi Muro alisema Mfuko una vitega uchumi vya muda mrefu ambavyo ni pamoja na
jengo la Golden Jubille Towers lenye ghorofa 21 ambalo ndio Makao Makuu ya PSPF, Jengo la PSPF Commerial
Towers ambalo lina ghorofa 35, jengo hili ni refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati.
Pia PSPF imewekeza katika ujenzi wa Chuo cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo cha Sayansi na
Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Mfuko pia umejenga nyumba kwa ajili ya kukopesha wanachama wake na watanzania wengine katika mikoa ya
Morogoro, Dar es Salaam, Shinyanga, Mtwara,Tabora na Iringa.
Baada ya semina hiyo wageni hao kutoka Clouds Media Group walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali
ya PSPF kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Mfuko huo na pia kutembelea baadhi ya maeneo ya uwekezaji wa
Mfuko.
Baada ya ziara hiyo, kiongozi wa timu kutoa Clouds Media, Bw. Kelly Michael alisema, “ ziara hii imetupatia elimu
ya kutosha juu ya PSPF…hakika kuna mengi tulikuwa hatuyajui lakini sasa tunaweza kumepata uelewa wa kutosha
juu ya Mfuko huu,”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...